Mganga Mfawidhi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mtwara – Ligula anakaribisha maombi ya kazi za kuijitolea kwa kada mbalimbali kama ilivyoahinishwa hapo chini:-
AFISA HABARI DARAJA LA II – NAFASI 1
SIFA ZA MWOMBAJI
Awe na Shahada ya Kwanza au Stashahada ya Juu ya Uandishi wa Habari au sifa inayolingana nayo kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali.
KAZI NA MAJUKUMU
- Kukusanya na kuandika habari.
- Kupiga picha.
- Kuandaa picha za maonyesho.
- Kuandaa majarida na mabango (Posters).
- Kukusanya takwimu mbalimbali.
- Kuandaa majarida na vipeperushi.
- Kuhifadhi picha na kuhudumia maktaba na marejeo.
FUNDI SANIFU VIFAA TIBA DARAJA LA II – (NAFASI 1)
SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa mwenye Stashahada ya kawaida ya ufundi (Full Technician Certificate) kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali.
KAZI NA MAJUKUMU
- Kufanya Matengenezo ya Vifaa vya huduma za tiba katika Hospitali za Wilaya.
- Kutunza kumbukumbu za kazi za kila siku.
- Kuinziza vifaa na vipuli vya kutengenezea Vifaa Tiba ngazi ya Wilaya.
- Kutunza Vifaa Tiba na vipuli.
- Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na Mkuu wake wakazi
DATA ENTRY (NAFASI 5)
SIFA ZA KUINGILIA
Kuajiriwa mwenye cheti cha kidato cha IV/VI, aliehitimu angalau stashahada katika fani yeyote kutoka Chuo kinachotambulika na Serikali
KAZI NA MAJUKUMU.
- Kukusanya fomu zote za BIMA Hospitalini.
- Kuchakata madai ya BIMA zote (kuingiza madai kwenye mfumo).
- Kuchakata makato ya BIMA zote.
- Kupokea na kuwasajili wagonjwa.
- Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na elimu, uzoefu na ujuzi wake
DEREVA (NAFASI 01)
SIFA ZA KUINGILIA
Kuajiriwa mwenye cheti cha kidato cha IV,awe na leseni iliyolipiwa daraja E au C1, Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya uendeshaji gari inayotolewa na Chuo cha mafunzo ufundi (VETA) au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali, awe na uzoefu wa miaka 3 bila kusababisha ajali,awe na cheti cha mjaribio ya ufundi Daraja la ll.
KAZI NA MAJUKUMU
- Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari Kuwapeleka Watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari.
- Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali.
- Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari “Log Book” Kufanya usafi wa gari.
- Kufanya kazi nyingine kadri atakavyoelekezwa na Msimamizi wake.
MORTUARY ATTENDANT (NAFASI 1)
SIFA ZA KUINGILIA
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne wenye cheti na uzoefu wa kazi za uhudumu katika chumba cha kuhifadhi maiti kwa muda usiopungua miaka miwili.
KAZI NA MAJUKUMU
- Kufanya usafi wa chumba cha kuhifadhia maiti.
- Kupokea kuosha na kutunza maiti
Kazi nyingine atakazopangiwa na kiongozi wake wa kazi.
MASHARITI YA JUMLA KWA WAOMBAJI
- Waombaji wote wawe ni raia wa Tanzania.
- Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.
- Waombaji wote waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detail CV) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
- Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya kidato cha nne na kidato cha sita kwa wale waliofika kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
- Viambatanisho hivyo vibanwe sawasawa kuondoa uwezekano wa kudondoka au kupotea:-
- Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificate
- Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI kwa waliofika kidato cha VI
- Vyeti vya kitaaluma (Professional certificate from respective boards) Leseni ya Uuguzi na Ukunga
- Picha moja “Passport size” ya hivi karibuni iandikwe jina kwa nyuma
- Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
Aidha atakaewasilisha barua yake kwa njia ya mkono ahakikishe anasaini kitabu maalumu cha kupokea barua hizi Masijala
Maombi yanaweza kuandikwa kwa lugha ya Kiswahili au Kingereza na yatumwe kupitia anuani ifuatayo:-
Mganga Mfawidhi,
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara,
S.L.P 520,
MTWARA
Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 04/09/2025 saa 9:30 Alasiri.